Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa AFCAFIM unaoratibiwa na IFAD wawezesha wakulima Kenya kuhimili mabadiliko ya tabianchi

Mfumo wa AFCAFIM unaoratibiwa na IFAD wawezesha wakulima Kenya kuhimili mabadiliko ya tabianchi

Pakua

Kwa miaka 45, mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo , IFAD umekuwa ukifadhili wakulima wadogo wadogo na maendeleo vijijini. IFAD inakuwa kama mratibu kwa kushirikiana na benki binafsi na sasa kuna mfumo wa fedha wa kuwezesha wakulima Afrika kukabiliana na kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi au ARCAFIM. Mfumo huo umewezesha kupatikana kwa dola milioni 700 za uwekezaji kutoka sekta binafsi kwenye kwa wakulima wadogo huko Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda, ili kutokomeza umaskini na njaa katika maeneo ya vijijini ya nchi zinazoendelea. Je, ni kwa jinsi gani wameweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi? Kupitia video iliyoandaliwa na IFAD, Pamela Awuori wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amefuatilia  mafanikio ya wakulima wadogo wadogo nchini Kenya, ungana naye. 

Audio Credit
Anold Kayanda/Pamera Awuor
Audio Duration
2'40"
Photo Credit
© FAO/Luis Tato