Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jean-Pierre Lacroix akamilisha ziara yake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR

Jean-Pierre Lacroix akamilisha ziara yake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR

Pakua

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix amekamilisha ziara yake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ambapo alikutana na walinda amani na kufanya mikutano na viongozi wa kijeshi. Taarifa iliyoandaliwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani CAR, MINUSCA..

Upsound

Nisalamu za kijeshi…… pamoja na gwaride maalum…… ikiwa ni kumkaribisha Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR.

Katika ziara hiyo Bwana Lacroix ameambatana na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini CAR, Valentine Rugwabiza, ambaye pia ni Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani CAR, MINUSCA.

Bwana Lacroix amesema kilichompeleka nchini humo ni kukutana na walinda amani Anasema …. “Nimekuja kuona wenzetu wapo mashinani wanavyofanya kazi, kuona maendeleo yaliyofikiwa katika kuboresha kambi, kujenga kambi mpya, kuhakikisha wafanyakazi wetu wanaume na wanawake wanakuwa na hali bora ya maisha, na pia kukutana na kikosi cha Ureno na Bhutan na kuwashukuru kwa kazi yao, kuwapongeza kwa yote wanayofanya, na kuwatakia mafanikio mema na, mwisho wa mwaka, wenye kheri na kuwaombe mema katika mwaka ujao, kwao na familia zao.”

Maafisa wengine walioambatana na Lacroix ni Jenerali Birame Diop, Jenerali Daniel Sidiki Traore na naibu wake Jenerali Pedro Miguel Alves Gonçalves Soares, pamoja na Kamanda wa Kikosi Jumuishi cha Bangui, Brigedia Jenerali Alognime Takougnadi.

Audio Credit
Jongo Sudi
Audio Duration
1'50"
Photo Credit
UN Photo/Eskinder Debebe