Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Changamoto la uhaba wa maji Turkana nchini Kenya laanza kupatiwa majawabu

Changamoto la uhaba wa maji Turkana nchini Kenya laanza kupatiwa majawabu

Pakua

Janga litokanalo na mabadiliko ya tabianchi ni janga pia la haki za watoto, linasema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF. Shirika hilo linasema mabadiliko ya tabianchi yanajidhihirisha kwenye ukame, vimbunga, mikondo joto, mafuriko na magonjwa Vyote hivyo vinaathiri zaidi watoto. Tayari nchini Kenya, katika kaunti ya Turkana, UNICEF na wadau wametambua changamoto hiyo na wamechukua hatua kurejesha tabasamu si tu kwa watoto bali pia kwa familia zao kupitia miradi mbalimbali, huku shirika hilo likitoa wito kwa serikali ya Kenya kuendelea kupatia kipaumbele huduma za nishati ya kufanikisha huduma za maji, nishati kama vle ya jua na upepo. Thelma Mwadzaya anamulika kwa kina kilichofanyika katika Makala hii iliyoandaliwa na UNICEF

Audio Credit
Selina Jerobon/Thelma Mwadzaya
Sauti
4'27"
Photo Credit
UNICEF/Victor Wahome