Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampuni ya Kijerumani yatuzwa Uganda kwa uhifadhi wa mazingira

Kampuni ya Kijerumani yatuzwa Uganda kwa uhifadhi wa mazingira

Pakua

Umoja wa Mataifa unahimiza uhifadhi na ulinzi wa mazingira kama njia mojawapo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Hata hivyo ufanikishaji wa lengo hilo unapigiwa chepuo na lengo namba 17 la ubia wa kimataifa ambao unataka kuleta pamoja wadau mbalimbali ili kuunga mkono juhudi za kitaifa na kimataifa. Miongoni mwa vitendo vinavyosababisha uharibifu wa mazingira ni ukataji miti hovyo ambapo nchini Uganda, kampuni moja ya kigeni imeitikia lengo 13 na namba 17 kwa kujikita katika utetezi wa mazingira na ulipaji kodi hadi imepatiwa tuzo ya uhifadhi wa misitu. Je inafanya nini? Mwandishi wetu wa Uganda, John Kibego amehudhuria sherehe hiyo ya tuzo na kutuandalia makala yafuatayo.

Audio Credit
Siraj Kalyango/Anold Kayanda
Audio Duration
3'42"
Photo Credit
World Bank/Curt Carnemark