Wakimbizi na wahamiaji hawaji kudoea bali wana mchango mkubwa pia:Profesa Gurnah
Mwishoni mwa wiki kamati ya kimataifa ya tuzo ya amani ya Nobel yenye makao yake makuu nchini Norway iliwatangaza washindi wa tuzo ya amani ambapo waandishi wawili wa Habari walishinda kutokana na mchango wao katika kusongesha na kupigania amani.