Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

UN News

Mahojiano la Mbunge Neema Lugangira kutoka Tanzania kuhusu nafasi ya mbunge kwa umma

Uwepo wa wabunge wenye nguvu ni msingi imara wa Demokrasia kwani wawakilisha hao wa wananchi wanakuwa na uwezo wa kupitisha sheria, kutenga fedha kwenda kufanya kazi ya utekelezaji wa sheria na sera walizozipitisha na kuwajibisha serikali iwapo haijatenda yale wananchi wanayakusudia kwakuzingatia makundi yote kwenye jamii hususan walioko kwenye mazingira magumu. 

Wabunge pia wanajukumu la kuunganisha masuala ya nchi zao na masuala ya kimataifa na hivyo hupitia na kupitisha mikataba na maadhimio ili kufanya dunia iwe mahali salama na yenye kuwanufaisha wanadamu wote.

Sauti
8'51"