Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Pasipo na amani, Tanzania tunakwenda kuleta amani- Balozi Mahiga.

Tanzania imesema licha ya kupoteza askari wake kwenye operesheni za ulinzi wa amani, bado itaendelea kushiriki kwenye operesheni  hizo kwani inatambua kuwa bila amani hakuna maendeleo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Balozi Augustine Mahiga amesema hayo leo kwenye maadhimisho ya miaka 70 ya ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa huko Dar es Salaam, Tanzania huku akitanabaisha kuwa pasipo na amani ndio Tanzania inakwenda kuleta amani.

Sauti
4'39"