Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Hali ya elimu yamulikwa nchini Sudan kusini

Sudan Kusini , taifa changa linalokumbana na changmoto mbalimbali mojawapo ikiwa ni elimu ya msingi. Nchini humo sio ajabu kukutana na watu wenye umri wa makamu ambao hawajui kusoma wala kuandika. Nini kifanyike? Na je nini kinakwamisha mchakato wa elimu nchini humo?

Ungana Grace Kaneiya katika taarifa inayomulika hali ya elimu nchini humo.

Mwanamuziki wa Uchina, Lang Lang atangazwa kuwa Balozi Mwema wa Amani

Umoja wa Mataifa una balozi mpya wa amani. Jina lake, ni Lang Lang, mcheza kinanda maarufu kutoka Uchina.

 [Muziki]

Na huo, ni mdundo uitwao Chopin Waltz, uloendana na hafla ya kumsimika balozi mwema wa amani. Aliyemtangaza, ni Katibu Mkuu, Ban Ki-moon

 “Kwa furaha na fahari, namtangaza Lang Lang kama balozi mwema wa amani wa Umoja wa Mataifa. Lang Lang, hongera na nakutakia kazi njema kwa ajili ya amani ya dunia!”

Katika ujumbe wake, Bwana Ban alisema muziki una uwezo mkubwa wa kufungua mioyo na fikra za watu

Amani yamulikwa jimbo la Abyei

Wakati wajumbe wa baraza la usalama na amani la Muungano wa Afrika, AU wakikamilisha ziara yao katika jimbo la Abyei nchini Sudan jimbo ambalo limeshuhudia migogoro kwa muda mrefu. Wakati ziara hiyo ikijiri, wakuu wa mataifa mawili , Sudan na Sudan Kusini wamekutana katika mchakato wa kuhakikisha amani inarejea jimboni humo.

Ungana na Joseph Msami anayemulika mkutano huo uanotoa matumaini ya kufikia amani katika jimbo la Abyei.

Mchakato wa UNICEF waendeleza elimu ya watoto wa kike Niger

Katika eneo hili la kusini mwa Niger, elimu ya watoto wa kike bado inapata pingamizi kutokana na shinikizo la itikadi za kitamaduni. Asilimia 36 ya wasichana nchini humo huingia ndoa za utotoni kabla ya umri wa miaka 15.

Katika kujaribu kupunguza pengo lililopo kati ya watoto wa kike na watot wa kiume wanaokwenda shule, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limekuwa likiendeleza mchakato wa shule zinazojali na kuzingatia maslahi ya watoto, ambao unawapa moyo watoto kwenda shule, hususan wale wa kike.

Jamii asilia zataka kushirikishwa katika mipango ya maendeleo

Wakati mikutano mbalimbali ya jamii za watu asilia ikichukua kasi mjini New York, kilio kikubwa cha jamii hiyo ni namna miradi ya rasilimali asilia inavyoathiri watu hao hususani barani Afrika pamoja na mitizamo hasi ya serikali kwa kundihilo.

 Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa, mwenyekiti wa jukwaa la kimataifa la watu wa asili Paul Kanyinke Sena amesema ni muhimu jamii hizo zihusishwe katika kupanga mipango ya maendeleo itakayohusisha ardhi wanakoishi ili kupunguza migogoro inayoweza kuepukikwa.

Dawati la jinsia ni ishara ya ushirikiano kati ya UM na Tanzania:

Wiki hii ni wiki ya Umoja wa Mataifa ambapo tarehe 24 Oktoba ni kilele. Hiki ni kipindi cha kutambua mchango wa Umoja wa Mataifa katika  Maendeleo ya

Tanzania na tayari shughuli mbalimbali zinaendelea jijini Dar es Salaam. Je shughuli hizo ni zipi? Na mambo yapi Umoja wa Mataifa inajivuniaTanzania. Stephen Mhando wa UNHCR katika mahojiano yaliyorekodiwa na Stephanie Raison wa UN-Women amezungumza na Usia Nkhoma-Ledama wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa na anaanza kwa kuelezea shughuli husika.

Vikosi vya Afrika vyaimarisha amani Somalia

Wakati hali ya usalama ikiimarika nchini

Somalia vikosi vya ulinzi wa amani vinavyoshirikiana na vikosi vya muungano wa Afrika nchini humo , AMISOM, kikosi cha walinda amani kutoka Kenyakimeondoka nchini humo.

Kuondoka kwa kikosi hicho ni kutoa fursa kwa kingine ili kuendeleza mchakato wa uimarishaji usalama Somalia nchi ambayo kwa takribani miongo miwili imeshuhudia machafuko. Joseph Msami anasimulia katika makala ifuatayo.