Gurudumu la mabadiliko Somalia halirudi tena nyuma: Balozi Mahiga
Nchi ya Somalia imepongezwa na viongozi kadha wa kadha, akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ban Ki-Moon, kutokana na jitihada ambazo imepiga kwenye mabadiliko ya kisiasa.
Katika hali hiyo, viongozi hawa wametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuendelea kuiunga mkono Somalia, kwani bado inakabiliwa na changamoto za kibinadamu na za kiusalama. Tangu kuteuliwa kama Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia, Balozi Augustine Mahiga amefanya kazi kwa bidii kuhakikisha kwamba Somalia imefikia kwenye nafasi iliyoifikia sasa.