Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Kituo cha haki za binadamu Tanzania chalaumu kuvunjwa kwa haki za binadamu

Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania leo kimetangaza ripoti yake ya awali inayoangazia mwenendo wa haki za kibinadamu kwa nchi hii katika kipindi cha miezi sita iliyopita na kutaja kasoro kadhaa ikiwemo kushamiri kwa matukio ya ubakaji unawandama hasa wanawake na watoto wa shule pamoja na vyombo vya dola kuangukia kwenye lawama ya utumizi mabaya wa madaraka.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Wataalamu wa uvuvi barani Afrika wakutana Tanzania kujadilia sekta hiyo

Wataalamu kutoka sehemu mbalimbali barani afrika wameanza mkutano wao wa siku nne jijini dar es salaam nchini Tanzania kujadilia kile kinachoitwa uchumi wa uvuvi wa samaki ambao unaripotiwa kukua kwa kasi lakini ukiandamwa changamoto ya kushamiri kwa uvuvi haramu.

Kutoka DSM, George Njogopa ameandaa taarifa ifutayo inayoangazia mkutano huo ambao pia umejuisha wataalamu kutoka nchi za Ulaya.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Vyama vya Siasa Afrika vyakutana Tanzania Kujadilia Ufadhili wa Fedha

Makundi ya kisiasa barani afrika yameanza mkutano wa siku tatu nchini Tanzania kwa shabaha ya kujadilia nafasi ya vyama vya kisiasa pamoja na mwelekeo mpya wa ufadhili wa mafungu ya fedha.

Wajumbe kwenye mkutano huo ambao umefunguliwa na makamu wa rais Dr Gharib Bilal wanatazamia kumulika nafasi ya vyama vya siasa nanma vinavyoweza kushiriki kwenye ujenzi wa demokrasia na wakati huo huo kuwavutia wapiga kura katika mazingira ya amani na utulivu.