Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Shirika la kimataifa la uhamiaji linasaidia watu wanaokimbia machafuko Abyei

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan umesema wakati maelfu ya watu wakikimbia jimbo la Abyei Sudan kutokana na machafuko na kuelekea Sudan Kusini, mashirika ya misaada yanaongeza juhudi za msaada wa kibinadamu.

Jumbe Omari Jumbe , msemaji wa Shirika la kimataifa la uhamiaji (IOM) amezungumza na Redio ya Umoja wa Mataifa hii leo juu ya hali katika eneo la Abyei na juhudi za IOM kuwasaidia wale wanaokimbia  machafuko jimbo hilo la Sudan.

Serikalia ya mpito ya Somalia lazima iafikiane:UM

Serikali ya mpito ya Somalia imeambiwa sasa umefika wakati wa kumaliza tofauti zao, na kuzingatia maslahi ya taifa.

Wito huo umetolewa na ujumbe wa braza la usalama la Umoja wa mataifa uliohitimisha mkutano wa kujadili hali ya Somalia mjini Nairobi Kenya.

Ujumbe huo umetoa muda wa wiki kadhaa hadi katikati ya Juni kwa Somalia kufikiri, kujadili na kuamua hatma ya taifa lao kwa kuitisha uchaguzi na kumaliza kipindi cha mpito kama ilivyopangwa.

IOM kusafirisha mamia ya wahamiaji waliokwama jangwani Chad

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kuanzia mwishoni mwa wiki hii wataanza kuwasafirisha maelfu ya wahamiaji waliokwama jangwani mpakani mwa Chad na Niger.

Wahamiaji hao ni wale wanaokimbia machafuko Libya, na kujikuta wamekwama kwa kukosa urafiri wa kuwafikisha Chad. Kwa mujibu wa IOM wahamiaji hao wengi kutoka Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara watasafirishwa kwa njia ya malori na watakuwa na safari ngumu na ndefu ya zaidi ya siku 20 jangwani.

Suluhu ya Somalia ni kutekeleza muafaka wa kisiasa na kufanya uchaguzi:Mahiga

Somalia ambayo kwa zaidi ya miongo miwili sasa haina serikali kuu inazidi kujikuta katika njia panda ya kisiasa kwa mgawanyiko kughubika uhusiano baina ya Rais wa serikali ya mpito na spika wa bunge.

Kwa mujibu wa mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Somalia balozi Agustine Mahiga tofauti hizo zinazidisha adha kwa mamilioni ya wasomali waliochoka vita na wenye kiu ya amani ya kudumu.

Hali ya Wachad wanaokimbia machafuko Libya yanatia hofu:IOM

Shirika la kimataifa la uhamaijai IOM linasema kuwa maelfu ya watu wanazidi kukimbia mzozo nchini Libya kila siku huku wasiwasi ukiibuka kuhusu hali ya raia wa Chad wanaowasili kwenye miji ya jangwani ya Faya na Kalait.

Jumbe Omari Jumbe msemaji wa shirika hilo la IOM anafanua zaidi alipozungumza na Alice Kariuki wa Idhaa hii

(MAHOJIANO NA JUMBE OMARI JUMBE)