Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

30 Septemba 2020

Kulinda bayonuai ni jukumu la kila mtu kwa ajili ya kiazazi hiki na vijavyo asema Bi. Elizabeth Mrema Katibu Mtendaji wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya bayonuai. Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mradi ulioendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF umewezesha watoto kufungua mradi wao wa kuoka na kupika mikate, mandazi na kalmati na hivyo kuona angalau nuru ya maisha kwenye taifa hilo lililogubikwa na mizozo hususan mashariki mwa nchi. Na UNIFIL yakita kambi Beirut kusaidia kurejesha maisha ya mji huo mkuu wa Lebanon.

Sauti
13'22"

29 Septemba 2020

Tuna imani na UN, lakini ijitathmini nasi wanachama tujitathmini- Tanzania. Si haki kwa watu milioni 690 kulala njaa wakati chakula kinatupwa kila uchao yasema UN. Tunakufa kwa njaa. Tunahitaji chakula, Sudan Kusini walia baada ya mafuriko. 

Sauti
13'45"

28 Septemba 2020

UN huiona Tanzania kuwa ni nchi ya kimkakati katika kutunza mazingira. Hatutawatupa raia wa Sudan Kusini inasema UNMISS. Nilianzisha PsychHealth kuziba pengo la huduma za afya ya akili Zambia:Chiwele. 

Sauti
12'16"

25 Septemba 2020

Wiki ya kwanza ya viongozi wa ulimwengu kuhutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ikielekea kukamilika, viongozi wengi kutoka barani Afrika ambao tayari wamehutubia, wameonesha kupigia chepuo umuhimu wa mshikamano kwani hatua walizozichukua kitaifa na kikanda zimekuwa ndio chanzo cha bara la Afrika kuudhitibi ugonjwa wa COVID-19 kinyume na fikira za awali za baadhi ya watu kuwa ugonjwa huo ungewapukutisha watu wengi katika bara hilo linalokabiliwa na mifumo duni ya afya.  

Sauti
11'24"

24 Septemba 2020

Ni wakati wa kuwatambua mabaharia na wahudumu wengine wa meli kama wafanyakazi muhimu. Vijana wa Somalia wakutana kujadiliana kuhusu ushiriki wao kuiendeleza nchi yao. Biashara ya kunenepesha na kuuza kondoo yainua kipato cha familia Sahel.   

Sauti
11'54"

23 Septemba 2020

Tanzania haikuongozwa na mihemuko ya kisiasa katika kukabili COVID-19, asema Balozi Kennedy Gastorn, Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. Machafuko Cabo Delgado, Msumbiji; raia 1000 wa wavuka mto Ruvuma na kuingia Tanzania.Mafuriko yafurusha maelfu ya wakimbizi Niger.

Sauti
12'28"

22 Septemba 2020

Mjadala wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa UNGA75 wafungua pazia. Zaidi ya watu milioni 1 waelezea matumaini na hofu yao kuhusu mustakabali wa UN. Amal Jazz Band, bendi ya muziki inayoeneza amani Malakal, Sudan Kusini.

Sauti
14'28"

21 SEPTEMBA 2020

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea 

-Umoja wa Mataida waadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa mkuu wa Umoja huo asema pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana safari bado ni ndefu inayohitaji mshikamano kunusuru kizazi hiki na vijavyo

-Tanzania inasema katika miaka 75 ya Umoja wa Mataifa kumekuwa na ushirikiano mkubwa na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ikiwemo la maendeleo UNDP, na la utalii UNWTO utamsikia Devotha Mdachi kutoka bodi ya utalii Tanzania

Sauti
14'51"

18 Septemba 2020

Leo tukimulika mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA75 hususan maadhimisho ya miaka 75 ya Umoja wa Mataifa. Mwenyeji wetu leo ni mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Kennedy Gastony.

Sauti
12'31"

17 Septemba 2020

Watoto milioni 150 wa ziada wametumbukia katika umaskini kwa sababu ya COVID-19. Ikiwa leo ni siku ya usalama wa wagonjwa duniani, shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO limesema hakuna taifa linaweza kuwaweka salama wagonjwa wake iwapo linapuuza usalama wa wahudumu wa afya hasa wakati huu wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19. Machifu wa Oicha wasema mawasiliano ni muhimu kudhibiti machafuko DRC. 

Sauti
14'27"