Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

TANZABATT 7/Ibrahim Mayambua

Asante walinda amani wanawake kwa kutujali- Wanawake Beni, DRC

Katika maadhimisho ya siku ya walinda amani duniani hii leo, maudhui yakilenga wanawake walinda amani ni ufunguo wa amani ya kudumu, baadhi ya wanawake wakazi wa mji wa Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wameomba walinda amani wanawake kutoka Tanzania waendelee kuwaunga mkono kiuchumi na kijamii.

Mmoja wa wanawake hao ni Kassoki Vaytsora Nadine, Chifu wa Kata ya Matembo mjini Beni ambaye msingi wa maombi yake ni changamoto wanazozipata akizitaja kuwa ni:

Sauti
3'58"
TANZBATT 7

Mwanamke kuchagua kazi ni kujibagua- Sajini Bari Mwita

 SGTBaru Mwita Makaya ni miongoni mwa madereva na Fundi mwanamke ambaye amejizole Umaarufu Mkubwa ndani nja nje Ya Tanzania , ambaye kwa sasa ni Mlinda Amani dereva na fundi Pekee Mwanamke. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

Nchini Jamhuri ya Kidemokrsia ya Congo, DRC ambako walinda amani kutoka Tanzania wanahudumu chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa kwenye mji wa Beni, jimboni Kivu Kaskazini tunakutana na Sajini Bari Mwita.

Sauti
3'23"
TANZABATT 7/Ibrahim Mayambua

Walinda amani wanawake kutoka Tanzania wasema, "wanawake DRC wanafunguka zaidi kwetu kuelezea masahibu yao."

Kuelekea siku ya walinda amani duniani kesho Mei 29, siku ambayo mwaka huu inamulika wanawake walinda amani wa Umoja wa Mataifa na mchango wao katika ujenzi wa amani ya kudumu, tunamulika askari wanawake wa Tanzania. Wanawake hao walinda amani wanahudumu katika kikundi cha saba cha Tanzania, TANZBATT 7, cha kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO kama anavyosimulia Assumpta Massoi .

Sauti
2'13"
Unsplash/Macau Photo Agency

Pamoja na kuleta adha COVID-19 pia imenisadia silali njaa:Fundi Beatrice

Mlipuko wa virusi vya Corona au COVID-19 kwa kiasi kikubwa umeathiri kila nyanja ya maisha ya watu duniani kote ukiacha kwamba umesababisha mamilioni ya vifo lakini pia umeathiri uchumi na maisha ya kijamii.

Na athari hizo za kijamii ni pamoja na watu kupoteza pato la familia kutokana na kukpoteza ajira, watoto kushindwa kuhudhuria masomo na hata shughuli za ujasiriliamali kusambaratika hali ambayo imewafanya wengi kujikuta katika wakati mgumu kumudu maisha ya kila siku.

Sauti
2'48"
UNICEF/Vincent Tremeau

COVID-19 imebadili maisha ya familia yangu- Mwanahabari Kanyinda

Ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19, upo na chonde chonde tujikinge. Ni kauli ya mwandishi wa habari wa kujitegemea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC aliyoitoa baada ya kupona ugonjwa huo ulioenea katika mataifa 216 duniani. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta Massoi)

Mwanahabari huyo Dieunit Kanyinda mkazi wa mji mkuu wa DRC, Kinshasa alibainika kuwa na virusi vya Corona tarehe 13 mwezi uliopita wa Aprili ambapo alilazimika kulazwa hospitalini kwa siku 16.

Sauti
2'23"
FAO Tanzania

Kikundi cha Umoja ni Nguvu Kakonko chanufaika na mafunzo ya FAO

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania wamesaidia wakulima hususan wilayani Kakonko  mkoani Kigoma kupata mbinu bora za kilimo na kuondokana na kilimo cha mazoea na hatimaye waongeze mazao ili siyo tu kukabiliana na umaskini bali pia kutokomeza njaa. Assumpta Massoi hivi karibuni alitembelea mkoa wa Kigoma na kuandaa taarifa ifuatayo.

Katika kata ya Katanga, wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma, wanawake wa kikundi cha Umoja ni nguvu, wanapalilia shamba lao nyakati za asubuhi wakiwa na ari kubwa.

Sauti
2'52"