Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UNHCR/Stephen Ferry

Wavenezuela waendelea kumiminika nchi jirani licha ya madhila wanayokumbana nayo njiani

Wakati hali ya kisiasa na kiuchumi nchini Venezuela inazidi kuzorota raia zaidi wa Venezuela wanakimbilia mataifa mengine ya Amerika ya Kusini ambapo takriban raia milioni 4 wa Venezuala wameihama nchi yao. Kando na kuwepo hali mbaya ya usalama na ghasia pia kumeshuhudiwa ukosefu wa madawa, chakula na miundo msingi. 

Audio Duration
2'59"
© UNICEF Patrick Brown

Miundombinu ya maji katika nchi nyingi bado ni duni- Ripoti

Shirika la Afya Duniani WHO na kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoratibu masuala ya maji, UN-Water wametaka hatua za dharura zaidi za kuwekeza kwenye huduma za maji safi na salama pamoja na mifumo ya huduma za kujisafi. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Jason Nyakundi)

Wito huo unakuja wakati idara za kimataifa za maji zinakutana mjini Stockholm kwenye mkutano wake wa kila mwaka wakati wa wiki ya maji duniani kati ya tarehe 25 na 30 Agosti mwaka 2019.

Sauti
1'48"
UN Japan/Ichiro Mae.

TICADVII: Ushirikiano Afrika na Japan unaleta tija- Guterres

Akiwa huko Yokohama nchini Japan akihudhuria mkutano wa 7 wa Tokyo kwa ajili ya maendeleo ya Afrika, TICAD VII, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema analiona bara la Afrika kama bara lililosheheni fursa ambako pepo za matumaini zinavuma kwa kasi kuliko wakati wowote ule. Grace Kaneiya na ripoti kamili.

(Taarifa ya Grace Kaneiya)

Sauti
2'9"