Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UNHCR/Tom Pilston

Filamu "Capernaum" kuhusu wakimbizi na wahamiaji yashindania tuzo za Oscars 2019

Nadine Labaki, mwongoza filamu kutoka Lebanon ambaye filamu yake ya Capernaum imechaguliwa kushindania tuzo ya Oscar kwa mwaka huu wa 2019 katika kipengele cha filamu za lugha ya kigeni, amezungmzia kile kilichomfanya kuandaa filamu hiyo inayohusu madhila yanayokumba mamilioni ya watu duniani katika zama za sasa ikiwemo  ukimbizi na uhamiaji.

Sauti
1'38"
UNICEF México

Watoto 3,000 waingia Mexico kutokea Guatemala siku 14 zilizopita

Zaidi ya watu 12,000 wakiwemo watoto 3000 wameingia Mexico wakitokea Guatemala kati ya tarehe 17 mwezi huu hadi leo, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.

UNICEF imetoa taarifa hizo leo mjini New York, Marekani na Mexico City nchini Mexico baada ya ziara ya siku mbili kwenye eneo hilo iliyofanywa na  mkurugenzi wake wa mawasiliano Paloma Escudero.

Sauti
1'43"
UNHCR/Alessandro Penso

Timisoara, ni makazi ya muda ya wakimbizi walio njiani kuelekea nchi ya tatu.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na shirika la kimataifa la Uhamiaji IOM wanaendelea na harakati za kuwahamisha wakimbizi kutoka Libya ambao sasa wamekuwa wageni wa muda wa serikali ya Romania kwenye  kituo cha ETC kilichoko mjini Timisoara Romania .

ETC ni makazi ya muda ya wakimbizi walio safarini kusaka usalama katika nchi ya tatu.  Wakimbizi hao wanapelekwa nchini Norway kwa ajili ya kupatiwa makazi ya kudumu.

Sauti
1'36"
© UNICEF/UN0233181/Herrmann

Ebola bado ni tishio DRC na hasa kwa watoto:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema mlipuko wa Ebola unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, umeathiri kwa kiasi kikubwa watoto, huu ukiwa ni mlipuko wa 10 nchini humo na wa pili kwa ukubwa duniani. Kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo serikali shirika hilo linafanya jitihada kuhakikisha huduma , dawa na vifaa vinapatikana ili kunusuru maisha ya watoto.

Sauti
1'35"
UNICEF/UN0149422/Sokhin

Mauji ya watoto Tanzania yatutia hofu:UN

Umoja wa Mataifa nchini Tanzania ,umelaani vikali mauaji ya watoto 10 kwenye mkoa wa Njombe yanayosadikiwa kutokea kutokana na imani za ushirikina. Mratibu mkazi wa Umoja huo amesema wanashirikiana na serikali kuhakikisha chanzo kinabainika huku ukitaka wahusika kufikishwa kwenye mkono wa sheria na watoto kupewa ulinzi stahiki.

Sauti
1'34"
OSCE

WFP na FIFA waungana kuimarisha masomo na michezo shuleni

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP na shirikisho la soka duniani, FIFA wamekubaliana kutumia mpango wa mpira shuleni unaondesha na FIFA na ule wa mlo shuleni unaondeshwa na WFP, kuimarisha stadi za wanafunzi kama njia mojawapo ya kujenga jamii imara, endelevu na zenye ustawi. 

Msemaji wa WFP mjini Geneva, Uswisi, Herve Verhossel, akizungumza na waandishi wa habari hii leo amesema  FIFA inatambua kuwa mpango wa soka shuleni unalenga kufanya mpira uchezwe na watoto wa kike na wa kiume kupitia somo la elimu ya viungo na kuchangia katika elimu ya mtoto.

Sauti
1'41"
UNICEF/UN0274546/Herwig

UNICEF yatoa ombi la dola bilioni 3.9 kwa ajili ya kusaidia watoto milioni 41 duniani

Mamilioni ya watoto wanaoishi katika nchi zilizoathiriwa na mizozo na majanga wanakosa huduma muhimu za ulinzi na hiyvo kuweka usalama na mustakabali wao hatarini, limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudmia watoto, UNICEF huku likisema linahitaji ombi la dola bilioni 3.9 ili kusaidia katika shughuli zake kwenye majanga ya kibinadamu.

Sauti
1'42"
UN Photo/Kevin Jordan

Makaburi ya pamoja yabainika huko DRC

Zaidi ya makaburi 50 ya pamoja nay a mtu mmoja mmoja yamebainika kwenye eneo la Yumbi, jimbo la Mai-Ndombe nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kufuatia mauaji yaliyoripotiwa kwenye eneo  hilo  katikati ya mwezi uliopita wa Disemba. 

Mkurugenzi wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini DR Congo, Abdul Aziz Thioye amesema hayo baada ya kutembelea eneo la Yumbi, kufuatia ziara iliyoandaliwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO.

Sauti
1'23"