Hakikisha usalama zaidi ili wahudumu wa kibinadamu waweze kusambaza chakula Sudan - WFP
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limezitaka pande zinazohasimiana nchini Sudan kutoa hakikisho zaidi la usalama kwa shirika hilo ili liweze kusambaza msaada wa chakula kwa wananchi waliokimbia makazi yao na waliokwama katikati ya mapigano ili kuwanusuru watu
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno “MITONGO.”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii lleo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “MITONGO.”
Mwanafunzi Msumbiji: Iwe mvua iwe upepo mkali madarasa yetu ni salama
Kila mwaka, Msumbiji hukabiliwa na matukio ya hali mbaya za hewa kupindukia kama vile vimbunga na mafuriko, matukio ambayo husababisha uharibifu wa shule na hatimaye watoto kushindwa kujifunza.
Kamishna Mkuu wa UNHCR akiwa ziarani Ethiopia anasihi wasisahaulike wanaoikimbia Sudan
Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Filippo Grandi akihitimisha ziara ya siku tatu nchini Ethiopia ametoa wito kwa ulimwengu kuwasaidia watu wa Sudan wanaoikimbia nchi yao na kuingia Ethiopia ambayo ni moja ya nchi wenyeji wa wakimbizi na wakimbizi wa ndan
31 JANUARI 2024
Hii leo jaridani tunafuatilia ziara ya Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Filippo Grandi nchini Ethiopia na wakimbizi wa ndani nchini Sudan. Makala tunakupeleka nchini Msumbiji na mashinani nchini Kenya. Kulikoni?
Simulizi ya Islam Mubarak: Ndoto yangu ni kurejea nyumbani na kuishi kwa amani
Kutana na Islam Mubarak msichana mwenye umri wa miaka 21 ambaye vita mpya iliyozuka Sudan Aprili mwaka jana ilimlazimisha kufungasha virago na familia yake na kuukimbia mji mkuu Khartoum na sasa amekwama katika kambi ya wakimbizi wa ndani katika jimbo la El-Gedarif, lakini ndoto yake ni kurejea n