Methali ATANGAYE NA JUA HUJUA!
Katika kujifunza Kiswahili tunaelekea Zanzibar nchini Tanzania kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili visiwani humo, BAKIZA Dkt. Mwanahija Ali Juma akifafanua maana ya methali ATANGAYE NA JUA HUJUA!
Katika kujifunza Kiswahili tunaelekea Zanzibar nchini Tanzania kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili visiwani humo, BAKIZA Dkt. Mwanahija Ali Juma akifafanua maana ya methali ATANGAYE NA JUA HUJUA!
Jaridani na Assumpta Massoi-
Leo ikiwa ni Ijumaa ni mada kwa kina ambapo tunaendeleza makala ya homa ya ini, pia kuna habari kwa ufupi zikiangazia habari muhimu ya siku. Katika neno la wiki inachambuliwa methali Atangaye na jua hujua!
Siku ya kimataifa ya kukabiliana na usafirishaji haramu wa kibinadamu huadhimishwa kila tarehe 30 ya mwezi Julai. Mwaka huu ujumbe ni Manusura wa usafirishaji haramu binadamu wawe msingi wa kampeni dhidi ya vitendo hivyo.
shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limekuwa msaada mkubwa katika sekta ya afya nchini Zambia wakati wa ugonjwa wa Covid-19 nchini Zambia na hata kabla ya janga hili kuikumba dunia.
Kiwango cha utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19 nchini Bhutan huko barani Asia kimefikia asilimia 90 ya wananchi wote wenye umri wa kupatia chanjo hiyo.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umepatia mafunzo ya mbinu za medani na usimamizi wa vilipuzi sambamba na ufyatuaji wa risasi, maafisa na wanajeshi 652 wa vikosi vya jeshi la serikali, FARDC na jeshi la polisi kama njia mojawapo ya
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umepatia mafunzo ya mbinu za medani
Nchi ya Bhutan yafanikiwa kutoa chanjo kwa 90% ya watu wake wanaotakiwa kupata chanjo
Jaridani Jumatano 28, 2021
Hii leo huko nchini Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan amezindua kazi ya utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19.
Uwekezaji wa kupambana na ugonjwa wa homa ya ini wazaa matunda.
Hii leo nchini Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan amezindua kazi ya utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19 kwa yeye mwenyewe kupatiwa chanjo hiyo pamoja na viongozi wengine waandamizi wa serikali, huku akisisitiza juu ya usalama wa chanjo hiyo iliyowasili nchini humo m
Leo ni siku ya Homa ya ini duniani, Shirika la kimataifa la kufanikisha upatikanaji wa tiba nafuu, UNITAID ambalo ni shirika tanzu la shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO inaadhimisha maendeleo yaliyofanywa katika kufikia malengo ya kutokomeza ugonjwa huo.