UM walaani mashambulio mawili ya bomu Iraq
Mashambulio mawili ya mabomu kwenye mji mkuu wa Ira Baghdad, siku ya Jumapili yamelaaniwa vikali na Umoja wa Mataifa.
Mashambulio mawili ya mabomu kwenye mji mkuu wa Ira Baghdad, siku ya Jumapili yamelaaniwa vikali na Umoja wa Mataifa.
Mcheza filamu nyota wa Marekani na mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa Leonardo DiCaprio ni miongoni mwa washindi wakubwa katika tuzo za Academy mjini Hollywood zilizotolewa Jumapili usiku.
Kuelekea siku ya kimataifa ya wanawake ambayo huadhimishwa kila Machi nane, ambapo utekelezaji wa melengo ya maendeleo endelevu SDGs kwa kuzingatia usawa wa kijinsia unamulikwa, nchini Uganda wanawake licha ya kukabiliana na utamaduni kinzani wanajikwamua kiuchumi.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP limepata ufadhili wa kutosha wa kurejesha misaada ya chakula kwa wakimbizi wa Syria waliopo Jordan, Lebanon, Iraq na Misri hadi mwisho wa mwaka.
Hatushuhudii kurejeshwa kwa vita baridi, mizozo ya leo ni ya aina mpya na tunapaswa kuiangazie na macho ya kisasa, amesema leo Waziri wa mambo ya nje ya Ugerumani, Frank-Walter Steinmeier ambaye pia kwa mwaka huu ni Mwenyekiti wa Shirika la Usalama na Ushirikiano la Ulaya OSCE.
Watafiti mashuhuri kutoka taasisi muhimu za afya watakutana katika Shirika la Afya kanda ya Amerika, PAHO, kuanzia kesho Machi Mosi had Machi Pili, ili kujadili mahitaji muhimu katika kuunda ajenda ya utafiti katika mlipuko wa virusi vya Zika, na athari zake kwa afya.
Umoja wa Mataifa na wadau wake wanapanga kusambaza msaada wa kibinadamu kwa raia wapatao 154,000 wanaoshi kwenye maeneo yaliyozingirwa nchini Syria wakati ambapo mapigano yamesitishwa kwa muda.
Rais wa baraza kuu la Umoja wa mataifa Mogens Lykettoft ameonya dhidi ya mapungufu makubwa tangu kuundwa kwa Umoja wa Mataifa, yakiwemo baa la njaa, mauaji ya halaiki, na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anafuatilia kwa wasiwasi maendeleo chini Comoro tangu tangazo la tume ya taifa ya uchaguzi CENI, la matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais wa muungano wa nchi hiyo na awamu ya kwanza ya uchaguzi wa magavana wa visiwa vya Comoro K
Wiki hii, Kenya imewasilisha ripoti yake huko Geneva, Uswisi, kuhusu hali ya haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni mbele ya kikao cha 57 cha kamati ya makubaliano ya kimataifa juu ya haki hizo.