Hali ya usalama bado ni tete CAR; Mia Farrow ashuhudia
Huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, hali ya usalama inazorota lakini juhudi za Umoja wa Mataifa zinaendelea ili kusaidia waathirika wa mgogoro unaondelea nchini humo.
Huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, hali ya usalama inazorota lakini juhudi za Umoja wa Mataifa zinaendelea ili kusaidia waathirika wa mgogoro unaondelea nchini humo.
Siku chache baada ya Umoja wa Mataifa kutangaza tarehe 22 January mwakani ya kufanyika kwa mkutano wa pili wa amani kuhusu Syria huko Geneva, wakimbizi wa nchi hiyo walioko katika kambi nchini Lebanon wanaelezea madhila wanayokutana nayo.
Serikali ya Uganda ilitangaza ugunduzi wa mapipa bilioni 3.5 ya mafuta chini ya bonde la ufa la Ziwa Albert . Utafutaji wa mafuta unaendelea wakati moja na mandalizi ya kwanza kuyazalisha.
Wakati dunia ikiadhimisha mkataba wa watoto unaolinda haki za kundi hilo muhimu katika jamii, nchini Kenya, kama kwingineko duniani, visa vya ubakaji vinatajwa. Hata hivyo katikati ya wingu hilo la ukatili wa kingono kuna habari njema za kuwanusuru wahanga wa matuko hayo.
Taarifa zinasema maelfu ya wahamiaji kutoka Tanzania wamekwama mipakani huku hali ya wasiwasi juu ya majaliwa yao ikiibuka. Hii inafuatia zoezi la serikali ya Tanzania kuwaondoa wahamiaji hao katika zoezi lililotangazwa na kutekelezwa na serikali hiyo. Hivi karibuni.
Mambo sasa ni shwari nchini Sudan Kusini. Hii ni baada ya matukio ya muda mrefu ya uwizi wa mifugo hatua iliyosababisha mamalaka ya polisi nchini humo kuingilia kati na kutoa mafunzo maalum kwa raia juu ya namna ya kukabiliana na uwizi huo.
Wakati kikao cha kumi na tisa cha mkutano wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia kikielekea mwisho taarifa zinasema hali ni tete katika mijadala ambapo mabishano yameibuka kati ya nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea .
Dunia ikiadhimisha siku ya choo duniani leo Nov 19, 2013 baadhi ya nyumba bado hazina vyoo. Takwimu zinaonyesha kuwa watu zaidi ya bilioni 2.5 kote duniani hawana vyoo hatua inayoweza kusababisha matatizo ya afya kwao.
Hapa Umoja wa Mataifa, mwishoni mwa wiki iliopita katika kumbu kumbu ya kumuenzi na kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mwanariwaya nguli Chinua Achebe.
(Makala ya Chinua)
Mkutano wa nane uliwaokutanisha maspika wanawake duniani umemalizika mwishoni mwa juma mjini New York huku mjadala mkubwa ukiwa ni mkakati wa usawa wa kijinsia kuwa sehemu ya malengo endelevu ya milenia baada ya 2015.