Biashara ya hewa ya ukaa bado kitendawili, gesi chafuzi zinazidi na umaskini ni kikwazo: Tanzania
Tanzania inaendelea na jitihada za kupunguza makali yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi wakati huu ambapo jopo la kimataifa la Umoja wa Mataifa linalojadili mabadiliko ya hali ya hewa IPCC limetoa ripoti kwamba shughuli za binadamu ndio chanzo kikuu cha mabadiliko hayo.