Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

07 DESEMBA 2022

07 DESEMBA 2022

Pakua

Hii leo jaridani tuanamulika Upper Nile nchini Sudan Kusini na nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani tunakuletea ujumbe. Kuhusu ukatili wa kijinsia.

  1. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limesikitishwa na kuongezeka kwa mapigano katika jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini ambayo umesababisha takriban watu 20,000 kuyahama makazi yao tangu mwezi Agosti, baadhi yao wakilazimika kukimbia hadi mara nne ili kuokoa maisha yao huku mzozo huo ukiendelea.   
  2. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kwa kushirikiana na wadau wake kama shirika lisilo la kiserikali la CAJED (CONCERT D’ACTIONS POUR JEUNES ET ENFANTS DÉFAVORISÉS), wanaendelea na huduma kadhaa muhimu za ulinzi kwa watoto ambazo ni pamoja na utambulisho, matunzo na kuwaunganisha watoto na familia zao. 
  3. Makala tunakwenda nchini Kenya ambayo inaangalia matumizi ya teknolojia ya nyuklia katika kuongeza uzalishaji wa kilimo.  
  4. Na mashinani tutasikia ujumbe ya kwamba sote tunapaswa kuwa wanaharakati wa kupambambana na ukatili wa kijinsia, nani kasema??

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'53"