Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Manusura wa usafirishaji haramu binadamu Ethiopia wasimulia yaliyowasibu 

Manusura wa usafirishaji haramu binadamu Ethiopia wasimulia yaliyowasibu 

Pakua

Tarehe 30 mwezi Julai kila mwaka ni siku  ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usafirishaji haramu wa binadamu duniani. Umoja wa Mataifa unasema mwaka 2018 watu 50,000 walibainika katika 148 kuwa wamesafirishwa kiharamu. Asilimia 50 ya watu hao wanatumikishwa kingono ilhali asilimia 38 ni utumikishaji kwenye ajira. 

Ni kwa kutambua hilo shirika la kazi duniani, ILO linatekeleza mradi uitwao  Better Regional Migration Project, yaani mradi wa kikanda wa  uhamiaji bora kwa lengo la kuimarisha usimamizi bora wa uhamiaji Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika lakini pia kusaidia waliorejea nyumbani. 

Katika makala hii ya leo tutamulika basi simulizi za waliorejea nyumbani baada ya kuponea chupuchupu kwenye mikono ya wasafirishaji haramu na msimulizi wetu ni Anold Kayanda. 

Audio Credit
Leah Mushi/Anold Kayanda
Audio Duration
4'28"
Photo Credit
© UNICEF/Jim Holmes