Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siyo ulemavu wote unaonekana-Wataalam wa Afya

Siyo ulemavu wote unaonekana-Wataalam wa Afya

Pakua

Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya kimataifa ya walemavu na kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa “sio ulemavu wote unaonekana” ni bayana kuwa  watu wengi duniani wanaishi na ulemavu wa aina fulani ambao hauonekani ambao wakati mwingine unaweza kuchukuliwa kuwa labda tabia zao na hata watu hao kukumbwa na unyanyapaa katika jamii. Mara nyingi ulemavu unaozingatiwa huwa ule unaonekana kwa mfano ulemavu wa miguu, mikono au macho ingawa nao bado wanakumbana na changamoto nyingi. Mwandishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi amezungumza na wataalamu wa afya ambao wamefafanua kwa kina kuhusu ulemavu usionekana akiwemo Daktari Sajjad Fazel ambaye ni mtafiti nchini Canada na Daktari Romana Sanitas kutoka Dar es Salaam Tanzania. Kwanza ni Daktari Sajjad.

 

Audio Credit
Anold Kayanda/ Jason Nyakundi
Audio Duration
3'46"
Photo Credit
© UNICEF/Amminadab Jean