Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kauli ya wahenga kuhusu samaki ni dhahiri kwa Wanjuhi Njoroge

Kauli ya wahenga kuhusu samaki ni dhahiri kwa Wanjuhi Njoroge

Pakua

Wahenga walinena kuwa samaki mkunje angali mbichi kwani akikauka hakunjiki! Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa mwanaharakati wa mazingira nchini Kenya, Wanjuhi Njoroge ambaye hivi sasa suala la miti na mazingira ni jambo ambalo ni sawa na kusema linatiririka kwenye damu ya mwili wake. Wanjuhi ambaye mwaka huu alipata fursa ya kuhutubia jukwaa la vijana kuhusu tabianchi jijini New  York, Marekani alimweleza Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa au UN News Kiswahili jinsi ambavyo mapenzi yake katika upandaji miti yalianza tangu utotoni na hivyo hivi sasa anachangia katika kufanikisha lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu hatua kwa tabianchi.

Audio Credit
Brenda Mbaitsa
Audio Duration
4'20"
Photo Credit
UNnewskiswahili/Patrick Newman