Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lugha ya kityaba iko hatarini kupotea nchini Uganda

Lugha ya kityaba iko hatarini kupotea nchini Uganda

Pakua

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya lugha ya mama hii leo Umoja wa Mataifa umesema lugha na utofauti wake wa utambulisho, kuwasiliana, kushirikiana kijamii, elimu na maendeleo ni muhimu kwa ajili ya binadamu na sayari dunia. Hatahivyo kukua kwa utandawazi kumesababisha lugha nyingi kuwa hatarini kupotea na iwapo lugha inapotea basi utofauti wa utamaduni unapotea na hivyo kuathiri kiungo muhimu cha jamii hizo. Nchini Uganda lugha ya kityaba inakabiliwa na hatari hii ambapo jamii wenyeji wa lugha hiyo wanahofu kubwa na lugha yao, kulikoni? Ungana na John Kibego katika Makala ifuatayo.

Audio Credit
Grace Kaneiya/ John Kibego
Audio Duration
3'45"
Photo Credit
IOM/A. Deng 2018