Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ethiopia yaazimia kuondokana na DDT, UNEP yaipatia msaada

Ethiopia yaazimia kuondokana na DDT, UNEP yaipatia msaada

Pakua

DDT kemikali yenye sumu iliyolenga kuangamiza wadudu waharibifu wa mimea na hata wanaosambaza ugonjwa wa Malaria yaani mbu imebainikuwa pale inapotumika husalia ardhini na kuharibu siyo tu mazingira bali pia afya ya binadamu na Wanyama.

Tayari nchi nyingi zimepiga marufuku matumizi ya DDT ilhali zingine zikiona bado zina uwezo wa kuitumia bila madhara yoyote. Kwa zile ambazo zimeamua kuteketeza maelfu ya tani ya DDT, shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, limeamua kuzisaidia na miongoni mwao ni Ethiopia.

 Makala hii ya leo inamulika ni kwa vipi basi operesheni hiyo imefanyika kama anavyosimulia Siraj Kalyango.

Audio Credit
Grace Kaneiya/Siraj Kalyango.
Audio Duration
3'41"
Photo Credit
UN