Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

FAO/IFAD/WFP/Petterik Wiggers

Uganda yahaha kuinua uzalishaji wa bidhaa za mifugo

Katika juhudi za kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu au SDGs na kuinua uchumi wa taifa Uganda imeamua kuchukua hatua mathubuti katika sekta mbalimbali ikiwemo ya ufugaji. Hivi sasa kupitia ongezeko la uzalishaji wa bidhaa za mifugo kwa ajili ya mauzo nje ya nchi, Uganda imelivalia njuga suala la kuwekeza katika teknolojia za kisasa, wakati huu ambapo nchi za Ulaya na China zimefungua milango kwa kununua bidhaa za mifugo na kilimo kutoka Uganda.

Audio Duration
3'57"
WFP/Jean-Fidele Ebenezer

Wakimbizi waomba msaada kukuza kipaji cha usanii Uganda

Mizozo hufifisha ndoto za vijana wengi baada ya wao kulazimika kufungasha virago mara nyingi kwa ghafla kitu ambacho huvunja mawasilaino na hatimaye mahusiano kwani kila mmoja husaka hifadhi popote pale kuna usalama bila kujali marafiki na akraba zake.

Wengine hupoteza mali zao na kulazimika kuanza maisha mapya ya kutegemea wahisani.

Sauti
3'44"
MONUSCO/TANZBATT/Taji Msue

Mradi wa kuoka mikate unaofadhiliwa na UN umeokoa familia yangu:Bichuna

Mradi wa Umoja wa Mataifa wa kuwasaidia waathirika wa ukatili wa kijinsia na kingono (SEA) katika mizozo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, umeendelea kuleta nuru kwa wanawake wengi na familia zao DRC ambayo imeghubikwa na vita kwa miongo sasa. Maelfu ya wanawake wamepitia ukatili huo na wengine hata kukata tamaa hadi pale mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO na ofisi maalum ya miradi ya kuwasaidia waathirika wa SEA kuanza kufanya kazi.

Sauti
3'46"
UN News/Assumpta Massoi

Je wajua kuwa ukubwa wa ziwa Tanganyika unazidi kupungua?

Nchini Tanzania, Ziwa Tanganyika lililopo mkoani Kigoma lasifika kwa kuwa la pili kwa kuwa na kina kikubwa zaidi duniani. Hata hivyo, kina na ukubwa wa ziwa vinapungua kutokana na mabadiliko ya tabianchi na shughuli za binadamu. Miongoni mwa mashuhuda wa hali hiyo ni Bwana  Kassim Govola Mbingo ambaye ni mhifadhi mkuu katika makumbusho ya Dkt. David Livingstone mjini Ujiji mkoani Kigoma. Katika mahojiano yake na Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya  Umoja wa Mataifa anafafanua

Sauti
3'55"
UNDP video

Juhudi za kukabilana na ukimwi katika maeneo ya mafuta,Uganda

Mwingiliano wa jamii kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uhamiaji, mizozo na kusaka fursa za kiuchumi huchochea mambukizi ya ugonjwa wa ukimwi na Hepatitis B yani homa ya ini na magonjwa mengine ya zinaa kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya ulimwenguni WHO.

Tishio hili ni dhahiri nchini Uganda hususan katika maeneo ya mpakani yenye shughuli za uchimbaji wa mafuta ambapo kando na ukimwi kuna tishio la ebola kutokana na wimbi la wakimbizi wanaoingia kutoka  nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Sauti
3'56"
UN-Habitat/Julius Mwelu

Kijana kutoka Nairobi Kenya aupa kisogo uhalifu na sasa anajihusisha na utunzaji wa mazingira

Kutana na Fredrick Okinda ni mmoja wa vijana waliokuwa wahalifu sugu katika mtaa wa mabanda wa Korogocho ulio mjini Nairobi, Kenya. Kama wahenga walivyonena kufanya kosa si kosa kosa kubwa ni kurudia kosa. Amejifunza kutokana na makossa na kuamua kubadili Maisha yake na ya vijana wenzie waliopitia njia kama yake. Kwa sasa Fredrick ni kiongozi wa kikundi kwa jina Kombgreen Solutions kinachowaleta pamoja vijana walio katika uhalifu, kuwasaidia kubadili tabia na kushiriki katika huduma za jamii hasa utunzi wa mazingira.

Sauti
3'43"
UN News/ Jonatha Joram

Ninarejeleza bidhaa chakavu ili kusafisha mazingira na kuokoa viumbe hai-Jonatha Joram

Ikiwa imesalia takribani miaka kumi kufikia mwaka 2030 ambao umepangwa kuwa mwaka ambao malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs yatakuwa yametimizwa. Juhudi kote duniani zinaendelea kuhakikisha lengo hilo linafikiwa. Nchini Tanzania, msichana mbunifu Jonatha Joram anayeishi katika jiji la Dar es Salaam ameamua kushiriki katika utunzaji wa mazingira kwa kurejeleza bidhaa ambazo tayari zimetumika ili ziweze kutumika tena badala ya kutupwa na kuchafua mazingira. Katika mahojiano haya na Anold Kayanda wa UN News, Jonatha anaanza kwa kueleza anavyozifanya shughuli zake

Sauti
3'37"
UN-Habitat/Julius Mwelu

Wanawake wapigania nafasi katika sekta ya mafuta, Turkana Kenya

Katika eno la Turkana nchini Kenya shughuli za uchimbaji wa mafuta zimeshika kasi, lakini kama ilivyo sehemu nyingi duniani kuna baadhi ya kazi ikiwemo ya uchimbaji mafuta zimekuwa zikichukuliwa kama ni kazi za wanaume. Lakini kwa wanawake wa Turkana wanasema hapana , kila kazi inaweza kufanywa na kila mtu endapo fursa inatolewa na jitihada zinafanyika. Na  matakwa ya wanawake hao ni kuweza kushiriki katika sekta hiyo yenye manufaa kwani uhusisha uwekezaji wa mabilioni ya dola za kimarekani.

Sauti
4'7"