Tusipoelewana vyema, itakuwa ni mzozo kila wakati na watu wa asili- Bi. Mulenkei
Kila uchao Umoja wa Mataifa unapigia chepuo ahadi ya nchi wanachama 193 ya kutomwacha nyuma mtu yeyote katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, ahadi iliyopitishwa na nchi hizo mwaka 2015 jijini New York, Marekani. Ahadi hiyo inazingatiwa katika utekelezaji wa malengo yote 17 na jambo la msingi ni kwamba mtu yeyote bila kujali kabila, rangi, umri, jinsi au imani yake ya kidini au kisiasa, hapaswi kuenguliwa. Kama ni masuala ya afya, mazingira, elimu au uchumi basi ujumuishaji lazima uzingatiwe.