Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Mkimbizi anatafuta maisha - JJ Bola

Umoja wa Mataifa unaendelea kusisitiza kuwa mtazamo potofu kuhusu uhamiaji na wahamiaji umeendelea kukwamisha matumizi bora ya dhana hiyo kote ulimwenguni. Umoja huo unahimiza serikali zote kuenzi mbinu tofouti za kufanya uhamiaji uwe na manufaa kwa wote, maana wakimbizi wanaweza kuchangia katika uchumi ya nchi wanamoishi. Licha ya wito huo bado wakimbizi wengi bado wanapitia machungu wanapokuwa ukimbizini, kitu ambacho kinasababisha wengi kuwaza walikotoka na machungu walioyapitia.

Sauti
3'55"

Viwanda vidogovidogo vyalaumiwa kuchafua vyanzo vya maji

Maji safi na salama ni uhai wa viumbe vyote ulimwenguni ikijumuisha binadamu, wanyama na mimea. Lengo namba 6 la  malengo ya maendeleo  endelevu, SGD linazungumzia maji safi na salama kwa kila mtu ifikapo  ya mwaka 2030.

Katika migogoro ya kimazingira, viwanda vidogo na vikubwa vimekuwa vikilalamikiwa kuharibu mazingira kwa kujenga mifereji inayopeleka maji taka katika vyanzo vya maji au mito.

Sauti
3'55"

Ni wakati wa vijana kuamka na kupiga kelele

Ripoti ya hivi karibuni ya shirika la kazi duniani, ILO  inaonyesha kuwa soko la ajira kwa vijana katika nchi zinazoendelea hususan katika bara la Afrika, Amerika kusini na Asia kusini linazidi kusuasua kutokana na ukuaji mdogo wa uchumi katika nchi hizo.

Umoja wa mataifa katika ajenda 2030 ya maendeleo endelevu au SDGs , inazihimiza serikali,  mashirika na asasi za kiraia kuwekeza katika taaluma au miradi itakayowawezesha vijana kujikwamuwa na tatizo la ajira ifikapo mwaka2030.

Sauti
2'54"
PICHA:IOM/Muse Mohammed

Makala ya Assumpta Massoi kuhusu bendi ya wakimbizi huko Brazil.

Nchini Brazil wakimbizi kutoka maeneo 10 tofauti duniani kuanzia Afrika hadi Asia na Mashariki ya Kati wameungana ili kutumia lugha moja inayofahamika zaidi duniani kusuuza siyo tu roho zao bali jamii  inayowazunguza. Wanamuziki hawa wanatumia lugha ya muziki wakisema kuwa ndicho kinawapeleka walikotoka kwa sababu mbalimbali ikiwemo vitisho, mauaji au ghasia. Je wanafanya nini huko Brazili? Ungana basi na Assumpta Massoi katika makala hii iliyowezekana kufuatia usaidizi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

Sauti
4'3"

Paschal Masalu wa ElimikaWikiendi ahojiwa na Habari za UN

Vijana wana mchango mkubwa katika kusongesha ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu au SDGs . Hayo yamesisitizwa katika jukwaa la vijana la Umoja wa Mataifa 2018 lililokunja jamvi hii leo kwenye makao makuu ya Umoja huo New York Marekani. Vijana 700 kutoka nchi mbalimbali wamejadili jinsi gani washirikishwe na mchango wao katika kufanikisha azma hiyo ya Dunia. Miongoni mwa waliohudhuria ni kijana Paschal Masalu kutoka nchini Tanzania ambaye ni afisa mtendaji wa jukwaa la Elimikawikiendi nchini humo.

Sauti
3'43"