ICC yawasilisha ombi kwa Baraza la Usalama la hati za kukamatwa viongozi wa Hamas na Netanyahu wa Israel
Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, Karim Khan ametangaza leo Mei 20 maombi ya hati za kukamatwa viongozi wa Hamas na Israel kwa madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika eneo la Gaza.
Ni Karim Khan, Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mapema leo alipotangaza kwamba anawasilisha maombi ya hati za kukamatwa viongozi wa Hamas na wa Israel kwa majaji wa mahakama hiyo ambao ndio watakaotoa uamuzi wa kutolewa kibali cha kukamatwa.