Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

WFP/Falume Bachir

Wakazi wa Cabo Delgado nchini Msumbiji hatihati kukosa misaada ya binadamu iwapo WFP haitapatiwa fedha za nyongeza

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP linasema iwapo halitapokea fedha za nyongeza, litalazimika kusitisha msaada muhimu wa kibinadamu kwa wakazi milioni moja wa jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji ifikapo kilele cha msimu wa njaa mwezi Februari mwakani kutokana na ukata unaokabili. Leah Mushi na taarifa zaidi.

Sauti
2'39"
Unsplash/Matt Palmer

Watafiti msifungie tafiti zenu, chapisheni na sambazeni- Dkt. Chang'a

Mkurugenzi wa masuala ya utafiti na matumizi ya hali ya hewa kutoka Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania TMA Dr. Ladislaus Chang'a amesema ni vyema wataalamu wa Afrika wakaongeza kasi katika kufanya tafiti na kuzichapisha katika majarida ya kimataifa ili tafiti zao ziweze kutumika katika utungaji wa será za kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Dkt. Chang’a ameyasema hayo akiwa Sharm el-Sheikh nchini Misri kunakofanyika mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27

Sauti
2'57"
UNFCCC

Taka za plastiki zageuka lulu Haiti

Miradi mbalimbali ya kukabiliana na uchafuzi wa mazingira inasaidia kuifanya dunia kuwa sehemu salama. Nchini Haiti Shirika la Benki ya plastiki linaendesha mradi wa kukusanya plastiki ikiwa ni moja ya njia za kuboresha afya ya na pia ni chanzo cha mapato kwa wakusanyaji taka. Leah Mushi na maelezo zaidi.

Plastiki zinaharibu sayari yetu, zinapokusanywa na kutumika tena zinasaidia kukata mnyororo wa uharibifu wa mazingira na hii ni njia mojawapo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
2'49"
Benki ya Dunia/Bamidele Emmanuel Oladokun

Mabadiliko ya tabianchi yaweka njiapanda vijana Afrika kuhusu suala la kupata watoto

Takriban nusu ya vijana barani Afrika wamesema wanafikiria upya suala la kupata watoto ama la kutokana na mabadiliko ya tabianchi, kwa mujibu wa ripoti mpya ya matokeo ya kura ya maoni iliyoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF bakwa kuwahoji watu 243,512 duniani kote. Taarifa ya Flora Nducha inafafnua zaidi  

Sauti
2'55"
Unsplash/Ralph Messi

Gabon na safari ya kulinda tabianchi kwa mustakabli endelevu

Nchini Gabon,  Benki ya Dunia imerejesha matumaini kwa jamii za wavuvi ambao uvuvi ndio tegemeo kuu la kujipatia kipato wakati huu ambapo uvuvi haramu ulianza kuleta shaka, shuku na hofu miongoni mwa jamii lakini sasa hatua za pamoja za uvuvi unaojali mazingira umeleta amani. Thelma Mwadzaya na maelezo zaidi katika ripoti hii iliyofanikishwa na Benki ya Dunia.

Sauti
2'29"
© UNICEF/Sebastian Rich

Tutoe mguu kwenye kichochea mwendo kasi cha uharibifu wa mazingira- Katibu Mkuu UN

Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27 ukiingia siku ya pili hii leo huko Sharm el-Sheikh nchini Misri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewakumbusha viongozi wa dunia na wote wanaohudhuria mkutano huo kwamba suluhu ya changamoto ya mabadikio ya tabianchi iko mikononi mwao na wakati wa kuchukua hatua ni sasa kwani hakuna tena muda wa kusubiri. Flora Nducha na taarifa zaidi 

Sauti
3'15"
© UNICEF/Lisa Adelson

Ubunifu wa vijana Zimbabwe wawezesha wanafunzi kusoma wakati wa COVID-19

Janga la COVID 19 lilipotangazwa mwaka 2019 lilizua taharuki kila kona ya dunia lakini changamoto zilizoletwa na janga hilo zilikuwa fursa kwa vijana nchini Zimbabwe ambao walikuja na wazo la shule mtandaoni na Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP likawapatia fedha ili watekeleze wazo na kuwanufaisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. Tuungane na Evarist Mapesa wa Radio Washirika SAUT FM ya Mwanza Tanzania kwa ufafanuzi zaidi.

Sauti
2'42"
© UNICEF/Mulugeta Ayene

Bado baa la njaa lanyemelea Somalia, asema Michael Dunford Mkurugenzi wa WFP Pembe ya Afrika

Ukame uliolighubika eneo la Pembe ya Afrika kwa miongo minne mfululizo umesababisha changamoto kubwa kwa mamilioni ya raia wa Kenya, Ethiopia na Somalia nchi ambayo maeneo mengi yanakabiliwa na kutokuwa na uhakika wa chakula na hatihati ya kutumbukia kwenye baa la njaa. Mashirika ya misaada ya kibinadamu likiwepo la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP yako mstari wa mbele kuwasaidia watu wenye uhitaji hususani wa chakula. Flora Nducha na maelezo zaidi!

Sauti
2'