Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

14 MEI 2024

14 MEI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika ugunduzi na ukuaji uchumi. Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda, UNIDO ni sehemu ya wawezeshaji wa jukwaa la WEIF 2024 na mwakilishi wake amezungumza na mwenyeji wetu huko Manama Bahrain Assumpta Massoi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.

  1. Huko Gaza Wapalestina zaidi waliouawa kutokana na mashambulizi ya kijeshi ya Israel wakiendelea kutambuliwa na mamlaka ya afya ya eneo hilo, wasaidizi wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wameeleza tena kwamba kwa hakika katika ya watu 35 ambao wameshauawa, idadi kubwa ya wanawake na watoto. 
  2. Kufuatia tathmini za kina nchini Malawi na Msumbiji, Timu huru ya Tathmini ya Kukabiliana na Mlipuko wa Polio (OBRA) leo Mei 14 imependekeza kufikia ukomo wa mlipuko wa virusi vya polio aina ya 1 (WPV1) nchini Malawi na Msumbiji, kuashiria hatua muhimu katika mapambano dhidi ya polio katika eneo la Afrika. Kisa cha mwisho cha WPV1 katika Kanda ya Afrika, kilichohusishwa na aina hiyo ya polio kiliripotiwa katika Jimbo la Tete la Msumbiji mnamo Agosti 2022. Jumla ya wagonjwa tisa waligunduliwa nchini Msumbiji na nchi jirani ya Malawi, ambapo mlipuko huo ulitangazwa Februari 2022.
  3. Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa njia ya video leo amewaeleza viongozi wa kimataifa jijini Paris Ufaransa kwamba “Tunahitaji hatua ya haraka ili kumpa kila mtu, kila mahali ufikiaji wa  nishati safi ya kupikia.” Guterres amewasisitiza viongozi hao wanaoshiriki Mkutano kuhusu nishati safi ya kufikia barani Afrika kwamba, “Tunacho kichocheo cha mafanikio: Ramani yetu ya Kimataifa ya Ubadilikaji ulio wa haki na jumuishi kuelekea nishati safi ya kupikia.”
  4. Mashinani tutaelekea nchini Somalia kufuatilia ziara za Bi. Catriona Laing, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia za kuwaaga viongozi nchini humo.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
11'35"