Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Francesco La Camera: Ushirikiano wa kimataifa utasaidia kuhamia haraka katika nishati jadidifu

Francesco La Camera: Ushirikiano wa kimataifa utasaidia kuhamia haraka katika nishati jadidifu

“Katika nchi zilizoendelea wanalazimika kubadilisha mfumo. Katika nchi zinazoendelea wao wanaweza kuruka na kwenda moja wa moja katika mfumo mpya wa nishati kwa kuwa hatuwezi kusema kuwa kuna mfumo halisi wa nishati ambao unafanya kazi huko. Kwa hiyo hii ndio tofauti kubwa, hali ya mfumo wa nishati katika sehemu hizi tofauti za dunia ambayo inaonekana kwa kiasi kikubwa katika ukosefu wa usawa uliopo. Hilo kwanza, la pili nchi zilizoendelea zinaweza kuwa vifaa, vyanzo fedha kufanya mabadiliko yatokee.”

Mkurugenzi Mkuu wa IRENA, Francesco La Camera (wa pili kushoto) akitembelea mradi wa umeme wa upepo unaofanywa na Jiji la Yancheng nchini China.
UN News/Jing Zhang

Akitoa mfano wa moja ya ushirikiano wa kimataifa unaoendelea hivi sasa Francesco La Camera anaeleza kuhusu ushirikiano wao na Kenya katika kusongesha matumizi ya nishati jadidifu barani Afrika akisema,

"Ushirikiano huu ulizinduliwa wakati wa mkutano wa Nairobi na kuwasilishwa katika COP28 mwishoni mwa kikao cha wakuu serikali, sasa tuna nchi saba za Kiafrika, ikiwa ni pamoja na Kenya. Kutoka upande w anchi zilizoendelea tuna Denmark, tuna Ujerumani, tuna UAE, na tuna Marekani. Na huu ni mfano wa namna tunavyojaribu kuandika upya namna ushirikiano wa kimataifa unavyofanya kazi. Tunasaidia nchi kujenga mpango wao. Na kisha kujaribu kubadilika pamoja kwenda nishati jadidifu katika muktadha wa ushirikiano wetu mpya wa kimataifa kutafsiri mipango kuwa ukweli.”

Shirika la kimataifa la nishati jadidifu, IRENA, linalojumuisha mataifa mbalimbali lilianzishwa tarehe 26 Januari mwaka 2009 ili kusaidia nchi duniani katika mabadiliko ya nishati, kutumika kama jukwaa la ushirikiano wa kimataifa, na kutoa takwimu na uchambuzi juu ya teknolojia ya nishati safi, ubunifu, sera, fedha na uwekezaji.

 

Pakua
Audio Credit
Leah Mushi/Anold Kayanda
Audio Duration
2'27"
Photo Credit
UN News/Jing Zhang