Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

20 MACHI 2024

20 MACHI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia hali ya huduma za afya katika ukanda wa Gaza, na harakati za chanjo kwa watoto nchini Yemen. Makala tunasalia huko huko Gaza na mashinani inatupeleka nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu siku ya furaha duniani.

  1. Wahudumu wa afya Gaza wanafanya kazi mchana kutwa na usiku kucha wakihaha kuokoa Maisha ya wagonjwa na majeruhi katika hospitali chache zilizosalia zikifanyakazi bila kutia chochote tumboni kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO.
  2. Katika kuhakikisha watoto wanapata chanjo zote zinazohitajika, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Yemen limekuja na mbinu ya kutumia watoto kuhamasisha jamii kupeleka watoto kupata chanjo. 
  3. Makala inatupeleka Gaza huko Mashariki ya Kati kupata taswira tofauti na ile ambayo imezoeleka kwa takribani miezi sita sasa. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi katika makala hii iliyoandaliwa na Ziad Talib, mwandishi wa Habari wa Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa huko Gaza.
  4. Katika mashinani ikiwa leo ni siku ya furaha duniani Sabrina Moshi wa redio washirika SAUT FM ya mkoani mwanza kaskazini magharibi mwa Tanzania ameuliza wananchi furaha ina maana gani kwao.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Sauti
11'52"