Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huku wanakimbia vita wanawake wa Gaza inakuwaje wakiwa katika hedhi?

Huku wanakimbia vita wanawake wa Gaza inakuwaje wakiwa katika hedhi?

Pakua

Kunapozuka mizozo na machafuko wananchi wote wanaathirika kwasababu maisha yao yanaparanganyika kabisa tofauti na walivyokuwa wamezoea. Watoto waliokuwa wakienda shule sasa hawaendi, si wafanyabiashara, wakulima wala viongozi wa dini wanaotekeleza majukumu yao ya kila siku na suala moja lililo kweli kwa kila mtu ni kuwa wanatafuta kila namna ya kuokoa maisha yao na wengi njia hiyo huwa ni kukusanya virango vyao kidogo wanavyoweza kubeba na kukimbia kuokoa nafsi zao. 

Kwa wananchi wa Gaza hususan wanawake wa Gaza, mwezi Oktoba mwaka 2023 mpaka leo wamekuwa wakikimbia mara kusini, mara kaskazini na sasa wapo Rafah karibu na mpaka wa nchi yao na Misri huku wengine wakiwa wamekwama maeneo mbalimbali ya ukanda huo kutokana na mapigano yanayoendelea baina ya wanamgambo wa kipalestina wa Hamas na jeshi la Israel IDF. Lakini ki baiolojia kila mwezi wanawake na wasichana waliovunja ungo huona siku zao au huingia katika hedhi , je wanawezaje kujihifadhi wakati huo huo wakiwa leo hapa kesho pale kuokoa nafsi zao? Tuungane na Leah Mushi katika Makala hii. 

Audio Credit
Flora Nducha/Leah Mushi
Audio Duration
4'35"
Photo Credit
UN News/Ziad Taleb