Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

29 JANUARI 2024

29 JANUARI 2024

Pakua

Hii leo kwenye Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa Anold Kayanda anaanzia na masuala ya afya, hususan viambato vya mafuta vinavyohatarisha afya ya mwili, kisha miradi ya UN ilivyosaidia wanawake huko Syria .Makala inakupeleka Angola kuona jinsi Umoja wa Mataifa umenusuru wanawake wa vijijini kwa hohehahe na mashinani atakupeleka katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko Kaunti ya Turkana, nchini Kenya kupata ujumbe kuhusu elimu hasa kwa wasichana.

  1. Kwa mara ya kwanza leo shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO, limezitunukia vyeti nchi tano kwa hatua kubwa zilizopiga katika kutokomeza viambato vya mafuta katika vyakula vinavyosindikwa viwandani kwa ajili ya kuongeza Ladha au Trans Fats. Flora Nducha amefuatilia taarifa hiyo na anatujuza zaidi.
  2. Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo FAO na la Mpango wa chakula duniani WFP yanasaidia kuinua maisha ya wananchi katika nchi ya Syria kwa kuwapatia miradi mbali mbali ikiwemo ya ufugaji wa kondoo. Leah Mushi anakusimulia kilichofanyika
  3. Makala Assumpta Massoi anakupeleka Angola, kusini mwa Afrika kusikia ni vipi mradi wa Umoja wa Mataifa umeheshimisha wanawake wa vijijini akiwemo mmoja wao aitwaye Albertina.
  4. Mashinani: Igiraneza Mixella, msichana mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye amesajiliwa kusoma kwa ufadhili wa Mpesa Foundation Academy ambayo huelemisha wanafunzi mahiri na wenye vipaji lakini wasiojiweza kiuchumi, akielezea jinsi alivyo na furaha isiyo na kifani kwa kutimiza ndoto zake za kuendelea na masomo yake ya sekondari katika shule hiyo.

Karibu!
 

Audio Credit
ANOLD KAYANDA
Sauti
11'44"