Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

12 JANUARI 2024

12 JANUARI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia kesi mbele ya mahakama ya Umoja wa Mataifa ya kimataifa ya haki ICJ inayotaka Israeli kukomesha mauaji ya raia huko Gaza, na haki za wanawake za unyonyeshaji. Makala tunakupeleka nchini Ukraine na mashinani nchini Kenya, kulikoni?

  1. Israel imekanusha vikali shutuma kuwa ina nia ya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina na kusisitiza kuwa ipo katika vita ambayo wao hawakuianzisha na wala hawakuitaka kufuatia hapo jana nchi ya Afrika kusini kuwasilisha kesi mbele ya mahakama ya Umoja wa Mataifa ya kimataifa ya haki ICJ wakitaka kukomesha mauaji ya raia huko Gaza.
  2. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF Rwanda kwa kushirikiana na wadau kama Shirika la Taifa la Maendeleo ya Mtoto nchini humo, NCDA, wanatoa wito kwa sekta binafsi, taasisi za serikali, washirika, asasi za kiraia kuweka mazingira rafiki ya unyonyeshaji mahali pa kazi. Evarist Mapesa anaangazia faida ya moja ya vyumba vya kunyonyeshea mahali pa kazi jijini Kigali Rwanda.
  3. Makala leo inakukutanisha na Olga mwathirika wa vita inayoendelea nchini Ukraine ambaye baada ya nyumba yake kushambuliwa na kombora mjini Borodyanka alikataa tamaa ya maisha lakini sasa mradi wa UNHCR wa kukarabati nyumba zilizoharibiwa na vita Ukraine umemfufulia matumaini ya Maisha yeye na mwanaye. 
  4. Mashinani inatupeleka Kakuma nchini Kenya ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula WFP limejenga ustahimilivu na uwezo wa kujitegemea miongoni mwa wakimbizi na jamii zinazowapokea, kupitia uzalishaji wa mazao na ufugaji unaohimili mabadiliko ya tabianchi”.   

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
12'14"