Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya ILO: Ukosefu wa ajira duniani kuongezeka 2024 sanjari na pengo la usawa

Ripoti ya ILO: Ukosefu wa ajira duniani kuongezeka 2024 sanjari na pengo la usawa

Pakua

Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa ILO kuhusu mtazamo wa ajira na kujamii imeonya juu ya kuongezeka kwa ukosefu wa ajira kimataifa kwa mwaka huu wa 2024, sanjari na pengo la usawa na kudumaa kwa kiwango cha uzalishaji hali ambayo inaibua wasiwasi. 

Ripoti hii ya mwaka 2024  iliyopewa jina Mienendo ya mtazamo wa Dunia wa ajira na kijamii 2024 imegawanyika katika sehemu kuu 4, mosi ni hali halisi ya mtazamo wa ajira duniani kote ambapo inasema ingawa kiwango cha ukosefu wa ajira na pengo katika kusaka ajira vilishuka kidogo chini ya kiwango cha kabla ya coronavirus">COVID-19  kutokana na mnepo uliojitokeza licha ya kuzororta kwa hali ya uchumi lakini matarajio ya kimataifa ndio yanayotia hofu kubwa.

Pili ripoti hiyo ya ILO imetaja nini kinachangia hofu hii kwa mwaka 2024, kwanza ni ongezeko la migogoro mipya ambayo mingi inapunguza matarajio ya kijamii ya kupata haki za kijamii ikiwemo ajira ikisema “Mwaka huu wa 2024 wafanyikazi milioni mbili zaidi wanatarajiwa kutafuta kazi, na hivyo kuongeza kiwango cha ukosefu wa ajira duniani kutoka asilimia 5.1 mwaka 2023 hadi asilimia 5.2. Mapato yanayoweza kutumika yamepungua katika nchi nyingi Tajiri duniani za G20 na, kwa ujumla, kuporomoka kwa viwango vya maisha kunaotokana na mfumuko wa bei ambao hauna uwezekano wa kutengamaa haraka".

Na pili ripoti inasema ni uwekezaji ambapo tofauti muhimu zinaendelea kati ya nchi za kipato cha juu na cha chini. 

Sehemu ya tatu ya ripoti ni nani waathirika wakumbwa ambapo imebainisha kuwa 

“Wakati kiwango cha pengo la ajira mwaka 2023 kilikuwa asilimia 8.2 katika nchi zenye kipato cha juu, kilisimama kwa asilimia 20.5 katika kundi la watu wenye kipato cha chini. Vile vile, wakati kiwango cha ukosefu wa ajira cha 2023 kiliendelea kuwa asilimia 4.5 katika nchi za kipato cha juu, kilikuwa asilimia 5.7 katika nchi za kipato cha chini.”

Mwisho ripoti imeongelea kuendelea kwa umasikini hususani katika nchi za kipato cha chini kutokana na ushiriki katika soko la ajira na pengo la usawa ikisema imesema idadi ya wafanyakazi wanaoishi katika umaskini uliokithiri  ambao wanapata chini ya dola 2.15 kwa kila mtu kwa siku iliongezeka kwa takriban watu milioni 1 mwaka 2023.

Pia idadi ya wafanyakazi wanaoishi katika umaskini wa wastani wakipata chini ya dola 3.65 kwa siku kwa kila mtu iliongezeka kwa watu milioni 8.4 mwaka 2023. 

Imeonya kwamba ukosefu wa usawa wa mapato umeongezeka, na hii "vinaashiria hali mbaya kwa mahitaji ya jumla na kujikwamua kuliko uendelevu zaidi kiuchumi.” 

Na katika ushiriki imesema ukosefu wa ajira kwa vijana umeendelea kuwa mtihani mkubwa hasa kwa wasichana na licha ya maendeleo ya teknolojia bado hakuna ongezeko lenye tija la ajira.

Mkurugenzi mkuu wa ILO Gilbert F. Houngbo amesema “Inaanza kuonekana kana kwamba kukosekana kwa usawa huku si sehemu tu ya kujikwamua na janga la COVID-19 bali ni suala la kimuundo. Changamoto za wafanyakazi inazotambua ni tishio kwa maisha ya watu binafsi na biashara na ni muhimu kuzishughulikia kwa ufanisi na haraka.”

Amesisitiza kuwa “Na bila uadilifu mkubwa wa kijamii kamwe hatutakuwa na ahueni endelevu”.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
2'47"
Photo Credit
© UN News/Daniel Dickinson