Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

10 JANUARI 2024

10 JANUARI 2024

Pakua

Jaridani leo tunaangazizia ripoti ya ajira ulimwenguni kote, na masuala ya afya nchini Botswana. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Afrika Kati, CAR. Mashinani tunaelekea Zanzibar nchini Tanzania, kulikoni?

  1. Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa ILO kuhusu mtazamo wa ajira na kujamii imeonya juu ya kuongezeka kwa ukosefu wa ajira kimataifa kwa mwaka huu wa 2024, sanjari na pengo la usawa na kudumaa kwa kiwango cha uzalishaji hali ambayo inaibua wasiwasi.
  2. Botswana iko njiani kutokomeza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI - VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, shukrani kwa msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya WHO kanda ya Afrika wakishirikiana na mashirika ya kiraia.
  3. Makala inakupeleka Jamhuri ya Afrika Kati, CAR ambako huko Umoja wa Mataifa umechukua hatua ya kukabiliana na habari potofu, za uongo na chuki kupitia redio. 
  4. Mashinani tunakuletea ujumbe wa mkulima wa mwani kutoka zanzibar nchini Tanzania kuhusu jinsi ufadhili wa Benki ya Dunia unavyoboresha ukulima wake.   

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
11'49"