Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

09 JANUARI 2024

09 JANUARI 2024

Pakua

Hii leo jaridani mada kwa kina tukimulika lengo namba 17 la Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs linataka uwepo wa Ushirikiano katika kufanikisha malengo. Ushirikiano huo unaweza kuwa baina ya nchi na nchi, wananchi na ushirikiano wa kikanda. Pia tunaangazia mzizo katika ukanda wa Gaza na Ukraine, na ripoi ya uchumi.

  1. Kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO na timu yake iliyoko huko idadi ya vifo na majeruhi Gaza kutokana na mzozo unaoendelea baina ya Israel na kundi la Hamas inaongezeka kila uchao na waathirika wakubwa ni wanawake na watoto.
  2. Ni karibu miaka miwili sasa tangu Urusi kuivamia Ukraine shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema wakimbizi zaidi ya milioni sita wamefurushwa kutoka makwao nchini Ukraine ambapo Zaidi ya wakimbizi milioni 5.9 wako katika nchi mbalimbali za Ulaya.
  3. Na ripoti ya Benki ya Dunia ya matarajio ya uchumi kwa mwaka huu iliyotolewa leo ambapo takwimu zinaonyesha kuwa huu ni nusu muongo uliodorora saana katika ukuaji wa pato la taifa au GDP kwa takribani miaka 30, huku matarajio yakionyesha kushuka kwa ukuaji wa uchumi duniani kwa mwaka wa tatu mfululizo kutoka asilimia 2.6 mwaka jana hadi asilimia 2.4 mwaka huu. 
  4. Mashinani tunarejea katika ukanda wa Gaza kusikiliza simulizi ya manusura wa vita baina ya Israel na kundi la Hamas.   

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
10'45"