Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

13 DESEMBA 2023

13 DESEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa COP28 ambao unafunga pazia leo. Pia tunamulika Kongamano la Kimataifa la Wakimbizi. Makala tunasalia huko huko Duabai kwenye mkutano wa COP28 na mashinani inamulika afya ya uzazi na haki za wanawake na wasichana walio katika mazingira magumu.

  1. Hatimaye mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28, leo umekunja jamvi mjini Dubai Falme za nchi za Kiarabu kwa muafaka ambao Umoja wa Mataifa unasema unatoa ishara ya kuanza kutokomezwa kwa mafuta kisukuku au fosil fuel ingawa baadhi ya nchi za visiwa vidogo vinavyoendelea ikiwemo Samoa zinaona muafaka huo hautoshelezi kuwalinda kikamilifu dhidi ya tabianchi.
  2. Ikiwa leo Kongamano la Kimataifa la Wakimbizi ambalo hufanyika kila baada ya miaka minne linaanza huko Geneva, Uswisi na kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo wakimbizi kutafuta suluhu na kuahidi hatua kwa ajili ya wakimbizi duniani na nchi na jamii zinazowahifadhi, nikepeleke sasa nchini Zimbabwe ambako kuna mfano wa wazi namna wakimbizi wanavyoweza kuwa na mchango chanya katika jamii zinazowahifadhi. 
  3. Makala inatupeleka Dubai, Falme za Kiarabu kwenye  mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28 ambako  huko Marynsia Mangu, Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la kiraia la Success Hands la nchini Tanzania linalohusika na kuwajengea watoto tabia ya kupenda kusoma vitabu ameshinda tuzo. Amezungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa baada ya kupokea tuzo na hapa anaelezea mengi ikiwemo alivyoipokea. 
  4. Mashinani itamulika afya ya uzazi na haki za wanawake na wasichana walio katika mazingira magumu.  

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Sauti
12'16"