Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

26 APRILI 2023

26 APRILI 2023

Pakua

Jaridani leo ripoti ya utalii wa milima na jamii ya watu wa asili wa Inuit.  Makala tunakuletea tunasalia hapa Makao Makuu na mashinani tunakupeleka Kisiwa cha Jamhuri ya Kiribati, kulikoni?

  1. Ripoti mpya iliyotolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau imeeleza bayana jinsi utalii kwenye maeneo ya milimani unaweza kuwa na manufaa sio tu kwa baiyonuwai bali pia kwa jamii zinazoishi kwenye maeneo hayo.
  2. Jamii ya Inuit ya watu wa asili wa Eskimo ni miongoni mwa jamii za walio wachache sana kutoka jimbo la Inuvik nchini Canada.
  3. Katika Makala Flora Nducha anazungumza na Kijana Mtanzania Gibson Kawago aliyeko hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa akihudhuria Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) la mwaka 2023.
  4. Na mashinani mashinani na tutaelekea katika Kisiwa cha Jamhuri ya Kiribati kilichoko Oceania katika Bahari ya Pasifiki ya Kati kusikia ujumbe kuhusu umuhimu wa chanjo.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Sauti
10'57"