Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MuDa Africa washindi wa ufadhili wa UNESCO wahamasisha wasichana kutoficha vipaji vyao

MuDa Africa washindi wa ufadhili wa UNESCO wahamasisha wasichana kutoficha vipaji vyao

Pakua

Wasanii kutoka Taasisi ya Muda Africa ya nchini Tanzania, kundi ambalo ni washindi wa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wanatoa wito kwa wasichana na wanawake kutoficha vipaji vyao ili waweze kutimiza ndoto zao na jamii iwasaidie kuyatimiza malengo hayo kwani hiyo itasaidia kuondoa pengo la usawa wa kijinsia katika tasnia mbalimbali ambazo kwa muda mrefu zinahodhiwa na wanaume. Wasanii hao wameyasema hayo hivi karibuni katika mazungumzo yao na Anold Kayanda wa Idhaa  ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa walipopata walipopata nafasi ya kutumbuiza wakati wa Mkutano wa nchi zenye maendeleo duni uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu wa Machi mjini Doha Qatar. 

Audio Credit
Selina Jerobon/Anold Kayanda
Audio Duration
4'4"
Photo Credit
UN News/Anold Kayanda