Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna wasiwasi kuhusu kesi dhidi ya Jaji Kisaakye wa Mahakama Kuu nchini Uganda - UN

Kuna wasiwasi kuhusu kesi dhidi ya Jaji Kisaakye wa Mahakama Kuu nchini Uganda - UN

Pakua
Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa majaji na mawakili Margaret Satterthwaite ameonesha wasiwasi wake mkubwa kuwa kesi za kinidhamu zilizoendeshwa dhidi ya Jaji wa Mahakama Kuu nchini Uganda Esther Kisaakye huenda zikawa sawa na kulipiza kisasi dhidi yake kwa kutekeleza majukumu yake ya kimahakama. Katika taarifa yake iliyotolewa kwa waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi hii leo Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa majaji na mawakili Bi. Margaret Satterthwaite amesema Jaji Esther Kisaakye mwaka 2021 alitoa uamuzi katika ombi la uchaguzi kati ya kiongozi mkuu wa chama cha upinzani Bobi Wine na Rais aliye madarakani Yoweri Museveni, uamuzi wa kumpa kiongozi huyo wa upinzani muda zaidi wa kurekebisha malalamiko yake ya kupinga matokeo ya uchaguzi.
Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
2'25"
Photo Credit
IMF/Esther Ruth Mbabazi