Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

30 JANUARI 2023

30 JANUARI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tuakuletea habari njema kuhusu afya na pia kuangazia jamii ya Benet nchini Uganda wakiwa bado hawana utaifa. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani tunasalia huko huko Kenya, kulikoni?

  1. Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, limesema mataifa mengi zaidi duniani yametokomeza magonywa ya kitropiki yaliyosahaulika, au NTDs huku ikisema bado uwekezaji zaidi unahitajika kusongesha maendeleo hayo dhidi ya magonjwa hayo kama vile ukoma, vikope na kung’atwa na nyoka.
  2. Baada ya zaidi ya takriban miongo minane ya kutokuwa na utaifa, jamii ya watu wa asili ya Benet nchini Uganda inahaha kuishi, na kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR bila kuwa na nyaraka rasmi muhimu jamii hiyo haiwezi kupata huduma za msingi kama elimu na afya , na sasa jamii hiyo inaiomba serikali ya Uganda kumaliza zahma hiyo iliyowaghubika kwa miongo.
  3. Makala tunakupeleka Kenya ambako huko mwandishi wetu Thelma Mwadzaya anamulika faida ya kuwa na kiwanda cha kutengeneza chakula lishe au tiba lishe kwa ajli ya watoto wenye utapiamlo uliokithiri.
  4. Katika mashinani tutasalia huko huko nchini Kenya kusikia ni jinsi gani wakimbizi wa Dadaab na wenyeji wameendelea kusihi pamoja kwa amani.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'