Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

12 DESEMBA 2022

12 DESEMBA 2022

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia amani na usalama nchini Yemen na DR Congo, Makala tunakupeleka nchini Msumbiji na mashinani tunakwenda nchini ya Sudan Kusini, kulikoni?

  1. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema watoto zaidi ya 11,000 nchini Yemn wameuawa au kujeruhiwa hadi kufikia sasa ikiwa ni sawa na wastani wa watoto 4 kwa siku tangu kushika kasi kwa machafuko nchini humo mwaka 2015.
  2. Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli ambaye ni Mkuu wa Utumishi katika Jeshi la Tanzania ametoa wito kwa Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kutanguliza majadiliano katika kutatua matatizo yao ya ukosefu wa amani.  
  3. Makala tunakwenda nchini Msumbiji kuangazia manufaa ya ushirikiano kati ya wabia wa maendeleo na wale wa usaidizi wa kibinadamu.  
  4. Na katika mashinani, nchi ya Sudan Kusini iliyoko Afrika Mashariki imeshika nafasi ya mwisho kwenye orodha ya vielelezo vya kuwa na mtazamo wa Rushwa kwa mwaka jana 2021. Wakiathimisha siku ya haki za binadamu mjini Juba nchini humo, Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kisiasa nchini Sudan Kusini Guang Cong na imeshauriwa nchi hiyo kufanya mageuzi haraka ili kushughulikia tatizo la rushwa.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
13'14"