Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

09 DESEMBA 2022

09 DESEMBA 2022

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia afya na waathirika wa ukame nchini Ethiopia. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Sudan Kusini.

  1. Utafiti mpya wa kisayansi uliofanyika kwa muda wa miaka sita umebaini kuna viwango vya juu vya usugu wa dawa dhidi ya vimelea au bakteria vinavyosababisha maambukizi kwenye mfumo wa damu yanayoweza kuhatarisha halikadhalika ongezeko la usugu w atiba dhidi ya vimelea vinavyosababisha magonjwa yaliyozoeleka kwenye jamii. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limesema hayo katika taarifa iliyotolewa leo jijini Geneva Uswisi. 
  2. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, James Cleverly akiambatana na Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Ethiopia, Gianfranco Rotigliano wametembelea eneo la Afar, nchini Ethiopia kujionea athari za ukame kwa watoto na familia na kutathimini hatua za dharura zizazochukuliwa na UNICEF ambapo Uingereza ni mdau muhimu kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa na muhisani. .  
  3. Makala leo tunakwenda nchini Kenya kumulika jinsi mradi wa maji uliofanikishwa na Umoja wa Mataifa umeleta ahueni kwa watoto na familia zao.
  4. Na mashinani wakati siku 16 za uhamasishaji kupinga ukatili wa kijinsia tutabisha hodi Gurei Juba nchini Sudan Kusini, kulikoni?

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Sauti
12'24"