Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

30 AGOSTI 2022

30 AGOSTI 2022

Pakua

Katika jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea 

-Nusu ya vituo vya huduma za afya duniani kote vinakosa huduma za usafi na hivyo kuwaweka wagonjwa na wahudumu wa afya katika hatari kubwa ya kusambaza magonjwa na maambukizi kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na WHO na UNICEF.

-Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la kuhudumia wakimbizi UNHCR, la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA na la mpango wa chakula duniani WFP yanaongeza juhudi zake za kuwasaidia zaidi ya watu milioni 33 wanaohitaji msaada baada ya kuathirika na mafuriko makubwa yaliyotokana na mvua za Monsoon nchini Pakistan.

-Meli ya Mv Ekarteria ambayo ni pili ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP iliyosheheni  tani 37,0000 za nafaka ya ngano imeondoka leo katika bandari ya Yuznhy Pivdennyi nchini Ukraine kupeleka msaada huo wa kibinadamu nchini Yemen ambapo kuna uhaba mkubwa wa chakula.

-Mada yetu kwa kilna hii leo inatupeleka Tanzania kwa mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la taia hilo BAKITA alitanabaisha wapi Kiswahili kilikotoka na kilipofikia hadi sasa

-Na mashinani tutamsikia msichana mtanzania ambaye amenuia kupeleka Tanzania, yale aliyojifunza nchini Marekani

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Audio Duration
12'56"