Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutawaelekeza maafisa ugani wetu wawasaidie wakulima Uyui, Tabora - Kosare Makori

Tutawaelekeza maafisa ugani wetu wawasaidie wakulima Uyui, Tabora - Kosare Makori

Pakua

 

Kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi kusababisha ukame katika maeneo mbalimbali ya dunia, kusababisha kupungua kwa mvua za masika, baadhi ya wakulima wa  wilaya ya Uyui mkoani Tabora, nchini Tanzania wanasema hawajasazwa katika kukumbana na athari za mabadiliko hayo kwani hata mvua za masika walizokuwa wanazitegemea kukuzia mazao yao, zimekuwa za kusuasua. Kwa sababu hiyo wameamua kujikita katika kilimo cha muda mfupi katika bustani ndogondogo ili waweze kujikumu kimaisha  lakini bado wanakumbana na changamoto nyingine ikiwemo kukosa mbegu na pembejeo, na kulazimika kutumia sumu nyingi ambazo ni hatari kwa mazingira na afya.  Hamad Rashid wa Redio washirika Tanzania kidstime fm kutoka Mkoa wa Morogoro amesafiri hadi Magharibi mwa Tanzania Kata ya Ibelamilundi Wilaya ya Uyui Mkoa wa Tabora na kuzungumza na wakulima.

Audio Credit
Grace Kaneiya/Hamad Rashid
Audio Duration
3'37"
Photo Credit
FAO Tanzania