Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchakato wa kuomba makazi katika nchi ya tatu ukirejea tutafurahi sana - Wakimbizi Kyangwali Uganda 

Mchakato wa kuomba makazi katika nchi ya tatu ukirejea tutafurahi sana - Wakimbizi Kyangwali Uganda 

Pakua

Mlipuko wa coronavirus">COVID-19 ulififiza mambo mengi ikiwemo mchakato wa wakimbizi kuomba hifadhi katika nchi ya tatu ambapo huwa na matarajio makubwa kama maisha kuwa bora na upatikanaji wa kazi. Wakimbizi huwa na matarajio mengi kuhusu kupatiwa hifadhi katika nchi ya pili ya ukimbizi kutokana na simulizi wanazosikia kutoka wenzao waliowatangulia kwenda ng’ambo. Hata hivyo ndoto zao ziikuwa zimetiwa mashakani na mlipuko wa coronavirus">COVID-19 ambapo mchakato wa kuomba hifadhi ulisitishwa. Wakimbizi akiwemo Madivan Ndayambaze aliyeko katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali nchini Uganda anasema hajavunjika moyo hasa wakati huu uchumi umeanza kufunguliwa. Maelezo zaidi yako katika mahojiano haya ya John Kibego na wakimbizi hao. 

Audio Credit
Anold Kayanda/John Kibego
Audio Duration
3'48"
Photo Credit
UN News/ John Kibego